Mchezaji wa zamani wa Liverpool Raheem Sterling amejiunga na kikosi cha Manchester City baada ya kupambana kwa muda mrefu kuihama klabu hiyo kwa madai kwamba anahitaji kucheza kwenye timu ambayo anaweza kutwaa mataji. Liverpool imekuwa na ukame wa mataji kwa miaka ya hivi karibuni, msimu uliomalizika ‘majogoo wa jiji’ walimaliza wakiwa nafasi ya sita wakiwa na pointi 64 na hiyo inamaanisha hawana nafasi ya kushiriki michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya ambayo kila mchezaji anatamani kucheza.
Sababu kubwa ya Sterling kuikacha Liverpool ni ukame wa mataji unaoiandama klabu hiyo, nyota huyo wa kimataifa wa England anaamini kuwa kwa sasa yupo kwenye kiwango bora hivyo anahitaji kuwa kwenye klabu itakayomuwezesha kutwaa vikombe.
Kuna wachezaji wengi ambao waliondoka Liverpool miaka ya hivi karibuni na wakafanikiwa kutwaa makombe ikiwemo la UEFA Champions League ambalo ndio kombe kubwa (lenye hadhi ya juu) kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.
Hii ni orodha ya wachezaji watano ambao waliondoka Liverpool kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kutwaa vikombe wakiwa na vilabu vingine.
Xabi Alonso-Real Madrid
Javier Mascherano-FC Barcelona
Alvaro Arbeloa-Real Madrid
Fernando Torres-Chelsea
Louis Suarez-FC Barcelona
0 comments:
Post a Comment