Wednesday, July 8, 2015

VIONGOZI wa TAIFA STARS SUPPORTERS wamefanya kikao cha kwanza kujadili mipango na malengo mbalimbali ya kundi hilo ambalo limeundwa mahususi kwaajili ya kuzipa hamasa timu zote za Taifa na kwa kuanzia walianza na mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda kule kampala.
Baada ya mechi hiyo ambayo Stars ilitoka sare ya 1-1 na kutupwa nje ya harakati za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa jumla ya magoli 4-1, kundi hilo linajipanga kuipa hamasa Tanzanite itakayochuana na Zambia Jumamosi Julai 11 katika uwanja wa Azam Complex.

Mbali na hilo, viongozi hao wamesema moja ya malengo yao makubwa ni Kusajili kundi hilo, kuhakikisha wanakuwa na katiba, kuhamasha na kusajili wanachama wengi kadri itakavowezekana kwa nchi nzima 

Aidha maazimio ya kikao hicho ni kuligeuza na kulisajili kundi kama chama cha washangiliaji kwa jina la chama cha washangiliaji Tanzania(TANZANIA FOOTBALL SUPPORTERS ASSOCIATION) .

Pia uzalendo huu hautoishia kwa timu za Taifa bali hata kwa vilabu vyetu vitakavokuwa vimepata uwakilishi wa taifa.
Azimio la tatu ni kuwa na jezi zetu za kututambulisha na azimio namba 4 ni kila mwanakikundi hai kulipa kiingilio cha 10000. Kiingilio hiki kitagawanywa katika sehemu kuu mbili.
1: 5000 kitambulisho
2:5000 itaingia kwenye mfuko wa/account ya group. Maazimio mengine ni kila mwanachama/ mwanagroup atatakiwa awe na kitambulisho na ili kupata kitambulisho atahitajika ajaze fomu na fomu mpaka jumamosi zitakuwa tayari yule atakae hitaji basi atatakiwa awe na passport size tatu.

Kwa sasa ofisi zao za muda zitakuwa kinondoni,   pale Meridian Hotel au Masai Club mpaka hapo watakapopata uongozi wa kikatiba.

Mwishoni kabisa mwenyekiti alifunga kikao muda wa saa 12 jion huku wakiazimia kukutana Ijumaa saa tisa pale Kebs Mwenge.

Viongozi wanawaomba wanagroup wote wavute subra kwa kipindi hiki ambapo viongozi tunapoendelea na vikao vya viongozi ili kufanya mambo mazuri kabla ya kukutana wote

Kikao cha jana kilianza mnamo saa tisa na dakika hamsini na moja na kilihuzuliwa na wajumbe saba 

1:Karigo Godson 
2:Yusuphed Mhandeni 
3:Ziota Musisa 
4:Haji Manara 
5:Amina Mohamed 
6:Dr Angelo Marcel 
7:Josephat Sinzo.

Wajumbe walimchagua mwenyekiti wa muda ndg Godson Karigo aweze kuendesha kikao. Wajumbe wote waliohudhuria waliazimia kuchagua uongozi wa muda utakao fanya mchakato wa baadhi ya mambo kuelekea ktk uchaguzi wa viongozi rasmi wa group hili.

Baada ya uteuzi wa viongozi wafuatao waliteuliwa:


1:Mwenyekiti: Yusuphed Mhandeni 
2: Makamu mwenyekiti wa kwanza: 
Haji Manara, 
makamu mwenyekiti wa pili: 
Ziota Musisa 
Makatibu wakuu Josephat Sinzobakwila na
Dr Angelo Marcel
Mratibu ni 
Madaraka Marumbo. 
Wajumbe ni 
1:Malkia (Amina Mohamed) 
2:Godson Karigo 
3:Asha Muhaj 
4:Maulid Kitenge 
5:Zena Chande 
6:Gerald Lukumay.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video