Baada ya klabu ya Simba kutangaza nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango wa timu ya Gor Mahia ya Kenya Boniface Oluochi, kipa huyo amesema amesikia tarifa hizo na yeye yuko tayari kujiunga na wakongwe hao wa soka la Tanzania na Afrika huku akiweka wazi kuwa anazimia sana kukipiga Msimbazi na kutoa sabu kadhaa za kuwazimia wakali hao ambao ni wapinzani wakubwa wa Yanga.
“Kusikia kweli nimesikia, waongee na timu yangu kama wao watamalizana mimi sina tatizo. Bado ninamkataba na Gor Mahia wa mwaka mmoja na miezi minne”, amlisema Oluochi.
Lakini golikipa huyo hakusita kutaja timu anayoizimia alipoulizwa ni timu gani angependa kucheza kati ya Simba na Yanga.
“Mimi napenda Simba. Kwasabaubu kuna wakenya wengi walishawahi kucheza Simba na wakafanya vizuri, ndugu yangu Jerry Santo alishawahi kucheza Simba. Simba ni timu kubwa na inaogopwa”, aliongeza.
Siku mbili zilizopita mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe alitangaza kuwa klabu yao inamuwania mlinda mlango wa Gor Mahia ambaye pia ni golikipa wa timu ya taifa ya Kenya Boniface Oluochi pamoja na mshambuliaji wa timu hiyo Michael Olunga.
0 comments:
Post a Comment