Monday, July 6, 2015

Klabu ya Simba imepata vijana 30 leo katika siku ya kwanza ya mradi uliopewa jina la Simba Vipaji kati ya vijana 123 waliojitokeza kuonyesha uwezo wao wa kucheza mpira kwa ajili ya kuunda timu ya vijana.
Mrad wa Simba Vipaji umeanza leo kwenye uwanja wa Mwenge Shooting jijini Dar-es Salaam chini ya kocha mkuu wa timu ya vijana Niko Kiondo, na unatarajiwa kutoa vipaji vipya vitakavyo jiunga na kikosi cha timu ya vijana Simba.
Katika mradi huu ambao unahusisha vijana wa miaka 15 – 18 kutoka ndani ya jiji la Dar-es salaam na mikoa ya jirani utafanyika kwa siku tano kuanzia leo tarehe 06/07/2015 mpaka 11/07/2015 kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wenye mapenzi ya dhati kwa Simba kutimiza ndoto zao za kuichezea klabu ya Simba.
Akizungumza na na simbasports.co.tz kocha Kiondo amekiri kupokea idadi kubwa ya vijana kutoka sehemu mbalimbali ambao wana vipaji na uwezo wa hali ya juu ya kucheza soka ,“kwakweli leo ni siku ya kwanza ila tumepokea vijana wengi kutoka sehemu mbali mbali zaidi ya 120 na tumefanikiwa kupata hawa 30 haikuwa kazi ndogo ukizingatia kwamba hii idadi yote walikuwa wana uwezo mzuri sana wa kucheza mpira”.
Simba Vipaji inatarajiwa kendelea tena kesho ikiwa ni siku ya pili huku ikitarajiwa idadi kubwa ya vijana kuongezeka. SIMBA NGUVU MOJA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video