Raheem Sterling ameiambia Liverpool kuwa hatarajii kuungana na klabu hiyo kwenda kwenye ziara ya kujiandaa na msimu ujao (pre-season tour).
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England anataka kulazimisha dili la kutimka Anfield na anaelewa kabisa akibaki England ataweza kufanikisha dili hilo kwa urahisi zaidi kuliko kama atasafiri na timu kwenda kwenye ziara Mashariki ya Mbali pamoja na Australia.
Manchester City wanatarajia kuipelekea Liverpool ofa nyingine ya tatu kwa ajili ya kumnasa kinda huyo mwenye miaka 20 huku Liverpool ikiwa imeshakataa pauni 35 ambayo ilikuwa ni ofa ya kwanza kutoka Man City, haikuishia hapo City ikaongeza na kupeleka ofa ya pili ya pauni 40 ambayo pia ilikataliwa wakati wao Liverpool wanataka walipwe pauni milioni 50 kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Sterling ambaye Jumatatu aliripoti Melwood (uwanja wa mazoezi wa Liverpool) kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao, anatarajiwa kuungana na kikosi cha Brendan Rodgers kitakacho safiri kuelekea Thailand siku ya Jumapili.
Mechi yao ya kwanza wakiwa ziarani itakuwa Bangkok Jumanne ijayo.a
0 comments:
Post a Comment