Hii ni habari mbaya kwa mashabiki wa Manchetser United wenye hamu ya kunasa kitasa hiki cha maana kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu England na mashindano mengine ikiwemo Uefa Champions League.
Stori ya kusononesha kwa mashabiki wa United ni kwamba,Sergio Ramos anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid na rasmi jaribio la Louis van Gaal kutaka kumsajili majra haya ya kiangazi linaelekea kufa.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwasasa yupo China ambako anatarajia kufanya mazungumzo na mlinzi huyo mwenye miaka 29.
Gazeti la Hispania la Marca, leo asubuhi limeandika stori hiyo ya usajili wa Ramos katika ukurasa wake wa mbele likiripoti kwamba Perez atalimaliza suala la Ramos kabla ya kurejea kupambana kumsajili David De Gea.
Ramos amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, lakini aliripotiwa kuwaambia Madrid kuwa anataka kutimkia Manchester.
Alhamisi iliyopita, Rafa Benitez alisisitiza kwamba Ramos kwa asilimia 100 haondoki Madrid, lakini kocha huyo alishindwa kukanusha jaribio lake la kuitaka saini ya De Gea.
0 comments:
Post a Comment