SAFARI YA MATUMAINI YA CHARLES MKWASA NCHINI UGANDA
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
CHAN 2016 QUALIFIER (Return Leg):
On Saturday, 4th July 2015
Uganda Vs Tanzania – (Uganda won 1st Leg 3-0)
Nakivubo Stadium, 4:00 p.m
Viingilio: 10,000/= (Ordinary), 20,000/= (Covered Stands) and 30,000/= (VIP) zote ni fedha za Uganda.
KOCHA mkuu wa muda wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesisitiza kuwa anaamini timu yake itapindua matokeo ya kipigo cha mabao 3-0 watakapoikabili Uganda kesho kwenye Uwanja wa Nakivubo.
"Mpira wa miguu ni mchezo wa makosa. Tunaweza kufunga mabao kama walivyofanya Uganda ugenini tukiwa nyumbani. Wachezaji wangu wanao uwezo huo na inawezekana.
"Tumeona ikitokea sehemu mbalimbali duniani. Miaka ya nyuma wakati ninacheza mpira, tulifungwa na Uganda 2-1 jijini Dar es Salaam, lakini tukashinda 3-0 jijini Kampala," amesema.
Mkwasa, kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga, ameyasema hayo muda mfupi baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, Uganda akiwa na kikosi cha Taifa Stars usiku wa kuamkia leo wakipitia Kigali.
Uganda itakuwa mwenyeji wa Taifa Stars kwenye Uwanja wa Nakivubo katika mechi ya marudiano kumalizia kibarua kilichobaki baada ya kushinda 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mechi ya kwanza.
Mkwasa alipewa jukumu la kuinoa Taifa Stars baada ya aliyekuwa kocha mkuu, Mdachi Mart Nooij, kutimuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kipigo kibaya dhidi ya Uganda.
Huku akiwatema beki wa pembeni kushoto mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, Edward Erasto Nyoni na kipa aliyekuwa chaguo la kwanza, Deo Munishi 'Dida', kocha huyo mpya Taifa Stars amesema kikosi chake kitawapa wakati mgumu Waganda kesho.
Maofisa waliokwenda na timu Kampala:
Charles Boniface Mkwas, Hemed Morocco (Assistant Coach), Omari Kapilima (Team Manager), Husein H.Swedi (Kits Manager), Peter Manyika (Goal Keeping Coach), Abdallah Kibadeni (Advisor), Martin Chacha (Ag. Competitions Director), Musa Amani Berenge (TFF Official), Ahmed Mgoyi (Coordinator) and Saloum Umande Chama (Head of Delegation)
0 comments:
Post a Comment