Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani amekumbana na adhabu ya kifungo cha kukosa mechi mbili baada ya tukio lililopelekea kutolewa nje kwa kadi nyekundu dhidi ya mchezaji wa Chile katika michuano ilimalizika hivi karibuni ya Copa America. Adhabu hiyo pia imemuangukia kocha wake Oscar Tabarez ambaye amefungiwa michezo mitatu.
Cavani alifungiwa kwa kumpiga kwa mkono mchezaji wa Chile Gonzalo Jara wakati wa robo fainali ya Copa America baada ya beki huyo wa Chile kumuingiza kidole sehemu za makalioni.
Wakati huo huo, Tabarez, alipewa adhabu ya kuondoka katika eneo lake baada ya kuigomea kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wake mwingine Jorge Fucile katika mchezo huo huo ambao ulimalizika kwa Uruguay kulala kwa bao 1-0.
Chama cha Soka nchini Uruguay sasa kimethibitisha rasmi kuwa Cavani ataukosa michezo ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 dhidi ya Bolivia na Colombia mwezi Oktoba.
Hii inaiacha Uruguay katika hali mbaya baada ya kuwa na pengo katika safu yake ya ushambuliji kutokana na mshambulizi wao mwingine tegemezi Luis Suarez kuwa bado anaendelea kuitumikia adhabu yake ya kushiriki michezo ya kimataifa baada ya tukio la kumng'ata beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa michuano ya kombe la dunia iliyofanyika mwaka jana chini Brazil.
0 comments:
Post a Comment