Wayne Rooney na mkewe Coleen wanatarajia kupata mtoto wao wa tatu, hii ni kwa mujibu wa Wayne Rooney mwenyewe.
Rooney ametangaza ujio hu wa kijacho wake kupitia akaunti yake ya Twitter jumatano usiku.
"Nina furaha kubwa sana kuwa mimi na @ColeenRoo tuko njiani kupata mtoto wetu wa tatu," Rooney ali-tweet.
Mtoto wa kwanza wa Rooney anayejulikana kwa jina la Kai Wayne Rooney, alizaliwa Novemba 2009, huku Coleen akimleta mwingine ambaye ni wa kiume anayejulikana kwa jina la Klay Anthony Rooney, Mei 2013.
0 comments:
Post a Comment