Christiano Ronaldo amekataa kuzungumzia hatma ya mchezaji mwenzake wa Real Madri Sergio Ramos alipokuwa akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha television.
Ronaldo hakusubiri mpaka mahojiano hayo yafike mwisho kwani baada ya kuulizwa juu ya hatma ya baadae ya mchezaji mwenzake Sergio Ramos, Ronaldo alisema; “Sifahamu chochote”, akazima kipaza sauti, akuvua ‘head phones’, akampa mkono mtangazaji na kuondoka.

Ramos ambaye inasemekana hana furaha kuwepo kwenye kikosi cha miamba hiyo ya La Liga kutokana na kutopewa thamani ndani ya klabu. Ramos amewaambia maafisa wa Real Madrid walitatue tatizo hilo mapema hadi kufikia Ijumaa kabla klabu hiyo haijaondoka kuelekea Australia na China kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu ujao (pre-season tour).
Ronaldo alifanyiwa mahojiano na kituo cha television cha SNTV mwishoni mwa juma hili na akazungumza mambo kadhaa juu ya Madrid.
“Sifahamu chochote”. Nyota huyo wa Ureno, 30, ghafla alikizima kipaza sauti chake baada ya mtangazaji kuanza kumhoji kuhusu masuala ya klabu ya Sergio Ramos.

Katika hali nyingine Ronaldo amesema anaamini rafiki yake wa karibu Ramos ataendelea kusalia Bernabeu na anaamini pia Real Madrid itafanikiwa chini ya kocha mpya Rafa Benitez.

“Real Madrid ni klabu kubwa sana duniani, kuna changamoto pia kuwa pale kama mchezaji au kocha”.
“Nitafurahi kufanya kazi pamoja nae. Tusubiri tuone kama tutashinda baadhi ya mataji muhimu. Na ninaamini juu ya hilo”.
0 comments:
Post a Comment