Mshambuliaji
inayeshinikiza kuondoka Liverpool, Raheem Sterling ametajwa kuwa ndiye mwenye thamani kubwa kwa wachezaji vijana
wenye umri chini ya miaka 21 barani Ulaya, huku wanandinga wengine watatu wa
England wakiingia kwenye orodha ya 20 bora.
Kwa mujibu
wa ripoti ya Soccerrex 20 U21, Sterling amepewa thamani ya
paundi milioni 35, ikiwa ni zaidi ya paundi milioni 7 za Marquinhos wa PSG
anayeshika nafasi ya pili.
Waingereza
wengine ambao wameingia kwenye orodha hiyo ni mlinzi wa kati wa Everton, John
Stones,
mlinzi wa
pembeni wa Manchester United, Luke Shaw na Calum Chambers wa Arsenal.
Hata hivyo,
kuna wachezaji wengine watano wa ligi kuu England katika orodha hiyo, ingawa
wawili kati yao hawajaanza kuzitumikia timu zao.
Nyota mpya
wa Manchester United, Memphis Depay mwenye thamanin ya paundi milioni 23.5
ameshika nafasi ya tatu, wakati mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi ambaye
msimu uliopita alicheza kwa mkopo klabu ya Lille ya Ufaransa ameshika namba 18
akiwa na thamani ya paundi milioni 10.7
Ripoti ya
Soccerrex 20 imezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kiwango cha klabu katika
ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa, thamani ya mchezaji kwenye soko la
usajili pamoja na uwezo wa sasa wa timu yake kuuza wachezaji kwa thamani kubwa.
ORODHA HII HAPA;
0 comments:
Post a Comment