Mlinzi wa
zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, mkongwe Rio Ferdinand
amemtumia ujumbe golikipa David de Gea ili asiihame klabu yake ya Manchester
United.
David de
Gea ambaye takribani miezi sasa amekua akihusishwa na kujiunga na miamba ya soka
nchini Hispania, Real Madrid.
Pamoja
na ukweli kwamba Manchester United hawajapokea ofa yeyote ya kiofisi kwa
mchezaji huyo lakini tetesi za chini chini zinasema golikipa huyo atatimkia
Madrid.
Rio Ferdinand
ambaye aliichezea klabu ya Manchester United kwa miaka mingi, amejikuta
akiishabikia timu hiyo na sasa hafurahii kuondoka kwa kipa huyo mhispania.
Katika
ukurasa wake wa Instagram, Rio alipost video iliyokuwa na maneno yake mwenyewe
na sauti ya wimbo uliosikika, 'please don't go' yaani tafadhali usiondoke. Huku
akitaja jina la David de Gea.
Ferdinand
anapata wasiwasi huenda lisemwalo likawa lipo na mara baada ya kumalizika
mchezo wa pili wa klabu yake ya Manchester United na San Jose Earthquakes, Rio
alitwiti kuuliza sababu za kutochezeshwa David de Gea.
Itakumbukwa
kuwa golikipa huyo amekataa ofa iliyopo mezani hivi sasa ya pauni 200,000 kwa
wiki aendelee kuitumikia klabu hiyo ya mjini Manchester.
0 comments:
Post a Comment