Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa na
wengi, moja ya nyota wa tenisi aliyekuwa akipewa nafasi ya kufika mbali kama si
kunyakuwa taji la Wimbledon ni Mhispania Rafael Nadal ambaye ameondoshwa
mashindanoni na mchezaji anayeshika nafasi ya 102 kwa ubora duniani, Dustin
Brown.
Brown ambaye ni mshiriki kutoka nchini Ujerumani
alimgaraza vibaya Nadal mwenye Grand slam 14 mpaka sasa kwa seti 7-6 3-6 6-4 6-4
na kuwaacha wapenzi wa mchezo huo midomo wazi wakiwa hawaamini kilichotokea
katika mchezo huo.
Brown alionekana kujiamini sana kutokana na kujua kuwa anacheza na
mchezaji wa kiwango cha juu na hata angepoteza isingeonekana kituko kwa wapenzi
wa mchezo huo duniani.
“Ilikuwa rahisi kwangu kucheza naye (Nadal) kwa sababu sikuwa
na cha kupoteza,” alisema Brown baada ya mchezo huo uliopigwa Usiku wa kuamkia
Julai 3.
Nadal ambaye ni bingwa wa Wimbledon wa mwaka 2008 na 2010,
alipangwa kukutana na Muingereza Andy Murray katika hatua ya nusu fainali, na
matokeo hayo yanaweza kuwa mazuri kwa Murray kwa moja ya ‘visiki’ kuondoshwa
mapema na hivyo kulainisha njia yake ya kuelekea kwenye fainali ya micuano hiyo
inayofanyika kwenye ardhi ya nyumbani.
Kipigo cha Nadal kutoka kwa wachezaji wanaoshika ‘namba za
viatu’ katika mchezo huo kinaonekana kama kitu kinachojirudia, kwani
alishapoteza kwa Lukas Rosol anayeshika nafasi ya 100 mwaka 2012 katika hatua
ya pili tu na baadaye kutandikwa na mchezaji anayeshika nafasi ya 135, Steve
Darcis mwaka 2013.
Kama hiyo haitoshi, mwaka jana kwenye mzunguko wa 4 alipokea
kipigo kutoka kwa mchezaji anayeshika nafasi ya 144 kwa ubora duniani, Nick Kyrgios
kitu ambacho wengi wanashangaa kwa nyota huyo.
Dustin Brown akishangilia kwa hisia baada ya ushindi dhidi ya Rafael Nadal |
Brown sasa atavaana na Mrusi mwenye asili ya
Serbia, Viktor Troicki
katika mzunguko wa 3 na wengi kusubiri kitu gani atafanya baada ya ushindi wa
kushtusha dhidi ya Mhispania Rafael Nadal.
0 comments:
Post a Comment