KOCHA Mkuu wa Yanga,Hans van der Pluijm, amepongezwa kwa uamuzi wake wa kuachana na kiungo kutoka Sierra Leone, Lansan Camara, aliyekuja kufanya majaribio na timu hiyo.
Wakizungumza na BINGWA baada ya mazoezi ya Yanga yaliyofanyika juzi asubuhi kwenye Uwanja wa Karume,Dar es Salaam,mashabiki wa timu hiyo walikiri kuwa Camara hana kiwango cha kutosha kusajiliwa na timu yao hiyo.
George Ndomba ambaye ni shabiki wa Yanga mkazi wa Keko, Dar es Salaam, alisema kuwa Camara hakuwa mchezaji mzuri wa kusajiliwa na timu yao.
“Camara ni mchezaji wa kawaida sana, hata hapa nchini wapo wa kiwango chake huko mitaani, angekuwa ni kocha mwingine angemsajili lakini Pluijm ameonyesha kuwa mtu wa mpira hasa na ndio maana ameachana naye,” alisema Ndomba huku akiungwa mkono na wenzake.
Aliwataka viongozi wa Yanga na klabu nyinginezo kuwa makini na wachezaji wa kigeni wasio na viwango wanaoletwa na wanaojiita mawakala kwa lengo la kujipatia fedha.
0 comments:
Post a Comment