Moja ya vifaa vinavyofanya kazi ya kuukarabati uwanja huo
Kutoka kushoto ni kaimu katibu mkuu wa chama cha soka IRFA, RAMADHANI MAHANO, meneja wa uwanja wa Samora LAZARO MANILA (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha soka IRFA CYPLIAN KUYAVA (Kulia)
Na Clement John, Iringa
Baada ya Shirikisho la soka nchini TANZANIA (TFF)kutangaza makundi na kipindi cha kuanza kwa ligi mbalimbali nchini kwa ngazi za vilabu ,chama cha soka mkoa wa Iringa kimeanza kuweka mikakati na mipango madhubuti kuhakikisha miundombinu inakuwa katika hali nzuri.
Siku ya Jumanne katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA-IRINGA) Mwenyekiti wa cham cha soka mkoa wa IRINGA, CYPLIAN KUYAVA alieleza kuhusu ukarabati wa eneo la kuchezea yaani(pitch) katika uwanja wa Samora ambao ulizinduliwa mwaka 1975 na aliyekuwa raisi wa nchi ya Msumbiji hayati SAMORA MACHEL.
Uwanja huo ambao hutumiwa na klabu za Lipuli ,African Wonderous ,Mtwivila city na klabu nyingine katika mkoa wa IRINGA umeanza kutolewa nyasi za zamani na kupanda nyasi mpya
Katika kuhakikisha zoezi hilo linakwenda sawa mdau mmoja wa soka mkoa mkoani IRINGA amejitolea kupanda nyasi ambapo nyasi hizo zitatoka nchini Afrika ya kusini na zoezi la upandwaji wa nyasi hizo mpya utaanza mara moja ,na inakadiriwa ni ndani ya muda wa wiki sita nyasi hizo zitakuwa zimeshika vizuri na matumizi yataanza.
Pamoja na jitihada hizo zinazofanywa na chama cha soka mkoa, nayo kampuni ya TANROADS mkoa wa IRINGA imeunga mkono ukarabati huo kwa kutoa mashine za kukwangua na kusawazisha eneo la kuchezea.
Kati ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na trekta na greda pamoja na shindilio la udongo na hivyo kurahisisha kazi hiyo
Kutokana na bili ya maji kuwa kubwa sana maji yatakayotumika kwenye umwagiliaji huo yatatoka kwenye kisima ambacho kipo uwanjani hapo, lakini vifaa kama mpira wa kumwagilia na pampu ya kuvuta maji kisimani tayari vimenunuliwa na chama cha soka.
Mwenyekiti wa chama cha soka amewaomba wadau mbalimbali katika mkoa wa Iringa kutoa mchango kwa klabu zitakazoshiriki ligi daraja la kwanza hapo baadae mwaka huu na ni klabu mbili za LIPULI FC na KURUGENZI zinazoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza (FDL)
0 comments:
Post a Comment