Baada ya kushinda kombe la Copa America akiwa na taifa lake la Chile, Alexis Sanchez bado hajarejea kwenye klabu yake ya Arsenal, kutokana na kuongezewa muda wa likizo na kocha wake Arsene Wenger.
Lakini hiyo haijamzuia Mchile huyo ambaye alishinda kombe la FA na Arsenal kufanya mazoezi ya kujiweka fiti tayari kwa kuanza msimu mpya wa ligi baada ya kuposti video akifanya mazoezi ya nguvu ufukweni.
Sanchez atakosa mchezo wa ngao ya hisani ambapo timu yake itakutana na Chelsea Agusti 2 na pia mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya West Ham Agusti 9.
Hapa akifanya yake kujiandaa na msimu mpya wa Ligi 'kazi kazi tu'
0 comments:
Post a Comment