Baada ya kuchukua ndoo ya Copa America Arturo Vidal hivi sasa anajiandaa kujiunga na Bayern Munich ambao wameshakubaliana kimsingi kumsajili mchezaji huyo kutoka Juventus.
Picha zilizotoka hivi sasa zinamuonyesha Vidal akiwa na kocha wake wa Chile Jorge Sampaoli wakiwa Miami kwa ajili ya mapumziko yao. Kitu ambacho kimewavutia watu wengi ni pale Vidal na kocha wake walipotumia sehemu ya muda wao kupasha misuli kwa kufanya jogging licha ya kuwa mapumzikoni.
0 comments:
Post a Comment