Wakati Mexico wakishangilia Ubingwa wa saba wa Mashindano ya Kombe la
Shirikisho la Soka la Nchi za MAREKANI ya Kaskazini na Kati pamoja na Visiwa
vya CARRIBEAN, CONCACAF GOLD CUP baada ya kuifunga Jamaica mabao matatu kwa moja katika Fainali iliyochezwa uwanja
wa Lincoln Financial Field, Marekani, nyota wa
zamani wa Tottenham na sasa LA Galaxy, Giovan dos Santos amesherekea kwa aina
yake.
Dos Santos ameweka picha kwenye mitandao ya kijamii
ikiwa na ujumbe unaowazodoa wenye chuki naye, huku akipiga kichwaji aina ya
Shampeni.
Mchezaji huyo ameenda mbali zaidi kwa kuweka pembeni
yake kombe la Gold Cup
0 comments:
Post a Comment