Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson akipokewa kwa heshima
Nyota wa Liverpool wamewasili Malaysia na kupokewa kwa heshima kubwa baada ya kutua mjini Kuala Lumper kumalizia ziara yao Austria na Mashariki ya mbali.
Brendan Rodgers na wachezaji wake wakiwemo nahodha Jordan Henderson, Adam Lallana na James Milner walivalishwa maua ya heshima baada ya kuwasili Saujana Resort kuelekea mechi ya kirafiki dhidi ya Malaysia XI itayopigwa siku ya Ijumaa.
Wekundu hao wa Anfield wamekuwa na kiwango kizuri katika mechi za maandalizi ya msimu kwani wameshinda michezo yote mitatu dhidi ya Thai All-Stars, Brisbane Roar na Adelaide United.
Wakimaliza mechi yao ya mwisho Mashariki ya mbali, wataelekea Finland kucheza mtanange mwingine wa kirafiki dhidi ya HJK Helsinki kabla ya kuhitimisha maandalizi ya msimu kwa kukupiga na Swindon Town.
James Milner
Wachezaji wa Liverpool na maafisa wake wakipiga picha ya pamoja baada ya kuwasili Kuala Lumpur
Mashabiki wa Liverpool wa Malaysia walijawa na furaha
Adam Lallana
Bendi ya asili ya Malaysia ikitumbuiza wakati Liverpool wamewasili
0 comments:
Post a Comment