Manuel Pellegrini amekiri kwamba Manchester City inatakiwa kufanya vizuri msimu huu ili kuepusha uwezekano wa Pep Guardiola kuvaa viatu vyake Etihad msimu ujao.
Pellegrini ameingia katika miezi yake
12 ya mwisho ya mkataba wake wa miaka mitatu baada ya msimu uliopita kumaliza bila kombe.
City walipokwa ubingwa na Chelsea na walitolewa na Barcelona raundi ya kwanza ya mtoano ya Champions League kwa mwaka wa pili mfululizo.
Pellegrini amesema ili kutunza kazi yake anahitaji kushinda makombe na kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa.
"Kitu cha kwanza ni kushinda makombe. Ni muhimu sana kushinda makombe-tutahitaji kushinda mataji yote manne na kufika hatua ya robo fainali ya Uefa Champions League". Amesema M-Chile huyo.
Ripoti za jana zinadai kwamba, Guardiola ameshafikia makubaliano binafsi ya kuifundisha Man City majira ya kiangazi mwakani.
Hiyo sio taarifa mpya kwani tayari kocha huyo wa Bayern Munich amekuwa kwenye rada za City kwa muda mrefu.
Guardiola amekataa kuongeza mkataba na Bayern na kuna uwezekano mkubwa wa kumrithi Pellegrini.
0 comments:
Post a Comment