Saturday, July 4, 2015

Baadhi ya Watanzania waliokuwepo kuishangilia Stars leo akiwemo Ally Yanga

Kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ chini ya kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa kimelazimisha sare ya kufungana goli 1-1 na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ mchezo uliomalizika muda mfupi kwenye uwanja wa Nakivubo jijini Kampala, Uganda ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrikakwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Goli la Stars liliwekwa kambani na John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Uganda kunawa mpira akiwa kwenye eneo hatari na mwamuzi wa mchezo kuamuru ipigwe penati, ndipo Adebayor alipoiandikia Stars goli hilo.
Lakini Uganda walisawazisha goli hilo dakika chache baadaye kupitia kwa Robert Sentongo baada ya mabeki wa Stars kutegeana kuondosha mpira kwenye eneo la hatari na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku Stars wakilishambulia kwa nguvu lango la Uganda ‘The Cranes’ ambapo dakika ya 18’ Simon Msuva alifunga goli lakini likakataliwa kwa sababu wakati anafunga goli hilo tayari alikuwa ameshaotea.
Simon Msuva, Deus Kaseke na Rashid Mandawa walifanya kazi nzuri kipindi chote cha kwanza wakigongeana pasi zilizowachanganya mabeki wa Uganda na kuifanya Stars kuonekana kuwa na nguvu mpaya chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa aliyeichukua toka kwa Mart Nooij aliyetimuliwa baada ya Stars kufungwa goli 3-0 Uganda kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, majuma mawili yaliyopita.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalika timu zote zilikuwa hazijafungana licha mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na imu zote mbili.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Stars wakiendelea kuliandama lango la Uganda kwa mashambulizi ya makali ambayo hayakuwapa nafasi ya kupumzika walinzi wa timu ya Uganda.
Ramadhani Singano ‘Messi’ aliingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva  wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Frank Domayo na Rashid Mandawa akapumzishwa kumpisha Salumu Telela.
Matokeo hayo  yanaifanya Stars kutupwa nje kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa goli 3-0 na leo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na kuwaacha Uganda kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya CHAN.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video