Monday, July 6, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KATIKA kile kinachoonekana Mbeya City FC hawana kubembeleza mchezaji, uongozi wa klabu hiyo ya Mbeya umeanika majina ya nyota 10 ambao hawakuwamo kwenye kikosi chao msimu huu.

Meneja Usajiri wa City, Frank Mfundo, amesema leo kuwa wachezaji hao ambao hawatakuwapo, wanatangulia idadi nyingine ya watakaoachwa mara baada ya mazungumzo kati yao na klabu kukamilika mwishoni mwa juma hili.

“Kwenye kikosi cha City msimu huu, Paul Nonga, Deus Kaseke,Peter  Mwalyanzi, Peter Mapunda, Fredy Cosmas, Idrisa Rashird, Lambony Luvanda Ashery, David Burhani, Anthony Matogolo na Deo Julius hawatakuwapo," amekaririwa meneja huyo katika mtandao rasmi wa City jana na kuongeza:
 
"Hii ina maana kuwa wameachwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuisha mikataba na hakukuwa na mazungumzo yoyote juu ya mikataba mipya, huku wengine wakiwa tayai wamejiunga na timu zingine."

Nonga na Matogolo wamejiunga na Mwadui FC, Kaseke amesajiliwa Yanga wakati Mwalyanzi ametua Simba.

Katika hatua nyingine, Mfundo amedokeza kuwa kuna wachezaji wengine kadhaa ambao bado wako kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu, hivyo taarifa ya mustakabali wao ndani ya kikosi cha City itatolewa  mwishoni mwa juma hili mara baada ya mazungumzo kukamilika.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video