Mshambuliaji hatari wa timu ya Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Michael Olunga baada ya jana kutupia goli mbili wakati timu yake ikicheza na KMKM na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 3-1, amesema kuwa bado kikosi chao kina kazi nzito ya kufanya licha ya kufanya vizuri mechi mbili za kwanza.
Olunga amesema lengo lao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kagame na kama wanataka kufanya hivyo basi wanatakiwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano hayo yanayoshirikisha vilabu bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Olunga ameingia kwenye rada za miamba ya kandanda Tanzania, Simba, Yanga na Azam FC.
Tetesi zinasema kwamba Yanga na Azam wanaitaka saini ya nyota, huku Simba wakithibitisha kwamba wametenga dola Elfu 20 kumsajili mkali huyo wa kucheza na nyavu.
Hata hivyo viongozi wa Gor Mahia wanasema kwamba timu inayotaka huduma ya Olunga inatakiwa kutoa dau la dola elfu 50 kwa klabu hiyo ili kuvunja mkataba, halafu wakae na mchezaji kujua anataka Shilingi ngapi.
0 comments:
Post a Comment