EMMANUEL Okwi, Laudit Mavugo anayetajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba na wengineo, wameonekana kumvuruga Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr ambaye ameshindwa kuanza programu yake kamili kutokana na kutokuwapo kwa nyota hao.
Okwi yupo nchini kwao Uganda kwa mapumziko ambapo alitumia nafasi hiyo kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Frolence Nakalegga mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati Mavugo yupo na timu ya Taifa ya Burundi inayokabiliwa na kipute cha michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Djibouti mwishoni mwa wiki hii.
Lakini pia, wapo wachezaji wengine wanaokwamisha programu ya Kerr waliopo timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Saidi Ndemla, Hassan Isihaka na Ramadhan Singano ‘Messi’ ambaye hata hivyo yupo kwenye mgogoro wa kimkataba na uongozi wa klabu hiyo.
Chanzo:Bingwa
Chanzo:Bingwa
0 comments:
Post a Comment