Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KIUNGO mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuondoka kwenda Denmark kufanya majaribio ya kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo, klabu ya Sonderjsyke.
Okwi; aliyeibeba Simba kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu uliopita, ataondoka lwenda Denmark kesho Jumanne Julai 7 kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa klabu ya Simba, Okwi amepata baraka zote za klabu hiyo ya Msimbazi kama ilivyosisitizwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva.
"Simba inajisikia fahari kuona Okwi amepata fursa hiyo ya kuonesha kipaji chake katika anga za kimataifa tena. Sisi, Simba, tunamtakia mafanikio na kila la kheri katika siku hizo 14 za majaribio katika klabu ya Denmark ya Sonderjsyke," amesema Aveva.
Hii si mara ya kwanza kwa Okwi kupata nafasi ya majaribio Ulaya kwani aliwahi kwenda Austria kujaribiwa na klabu ya Red Bull Salzburg.
0 comments:
Post a Comment