Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa Morgan Schneiderlin kutoka Southampton.
Usajili huu unakuja muda mfupi baada ya Mashetani hao wekundu kuthibitisha kumsajili Bastian Schweinsteiger kutokea klabu ya Bayern Munich.
Schneiderlin amesaini mkataba wa miaka minne Old Trafford,huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Ada ya uhamisho ya nyota huyo mwenye miaka 25 inaaminika kuwa ni paundi milioni 25.
Huyu ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Manchester United majira haya ya kiangazi kwani tayari wamenasa saini za Memphis Depay, Matteo Darmian na Schweinsteiger.
Usajili huu sasa unampa machaguo mengi Louis van Gaal katika safu ya kiungo kwani ana majembe mengine kama vile Ander Herrera, Michael Carrick, Daley Blind, Marouane Fellaini.
Akizungumza na Tovuti ya Man United Schneiderlin amesema ni jambo kubwa kuhama kutoka St Mary na kutua Old Trafford. He said:
"Nimefurahi sana kuwa mchezaji wa Manchester United. Nilipogundua kwamba United wanavutiwa na mimi, ilikuwa rahisi kuamua. Nimefurahia miaka saba niliyokaa Southampton, klabu hii wakati wote itakuwa moyoni mwangu. Laki nafasi hii ya kuwa sehemu ya kikosi cha timu kubwa (Man United) na kuipatia mafanikio nisingeipoteza".
Kocha wa United, Louis van Gaal amesema:
Ni mchezaji mwenye kipaji cha juu, ana nguvu na uwezo. Ujuzi wake utaendana na wachezaji wetu".
0 comments:
Post a Comment