Mkurugenzi Mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kumsajili rasmi Arturo Vidal.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Rummenigge amesema:
“Ninaweza kuthibitisha kwamba kimsingi tumefanikiwa kufikia muafaka kati yetu na Juventus pamoja na Vidal. Kilichobaki ni kupima afya na kusaini mkataba. Tunategemea mambo yataenda vizuri na haraka ili ajiunge na mazoezi ya klabu wiki ijayo”.
Vidal ameisaidia Juventus kucheza hadi fainali ya UEFA na pia timu yake ya taifa kuchukua kombe la Copa America.
0 comments:
Post a Comment