Na Ramadhani ngoda.
Licha ya ya kocha
Louis Van Gaal kuwa katika harakati za kuunda kikosi chake kwa kusajili na
kubakiza wachezaji muhimu katika kikosi chake, mlinda mlango aliyesajiliwa
msimu uliopita, Victor Valdes yupo katika mazungumzo na klabu ya Antalyaspor ya
Uturuki tayari kumaliza kipindi chake kifupi cha maisha ya United.
Uongozi wa
Antalyaspor umethibitisha kuanza mazungumzo na golikipa huyo na kama dili hilo
litakamilika, Valdes atakuwa mchezaji wa zamani wa 3 wa Barcelona kutimkia ligi
kuu nchini Uturuki baada ya Samuel Eto’o na Ronaldinho Gaucho kujiunga na timu
hiyo iliyopanda daraja msimu huu.
“Tupo kwenye mazungumzo
na Valdes. Kama makubaliano yakifikiwa, tutakuwa tumeweza kusajili mchezaji
mwingine wa hadhi kubwa duniani,” alisema ofisa habari wa klabu hiyo, Hassan
Ali Ceylan kukiambia kituo cha Eurospor TR.
Hili litakuwa ni pigo
kubwa kwa mabingwa mara 20 wa Uingereza kutokana na mlinda mlango chaguo la
kwanza, David De gea naye kuwa katika mlango wa kutokea Old Trafford na kurejea
katika nchi aliyozaliwa tayari kuwa mrithi wa Iker Casillas katika klabu ya Real
Madrid.
0 comments:
Post a Comment