Katika hali isiyokuwa ya kawaida, barua
aliyoandika kocha wa zamani wa Liverpool, mwenye historia kubwa, BILL SHANKLY akiomba
kustaafu mwaka 1974 imeonekana.
Akiaminika
kuwa ndiye kocha mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika soka la England, Shankly aliyefariki
dunia mwaka 1981 akiwa na miaka 68 aliifundisha
Liverpool kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 15 kabla ya kustaafu.
Nyaraka hiyo
imefichuliwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, JOHN ALDRIDGE katika
maktaba ya HOTELI YA SHANKLY na baada ya hapo akaandika kwenye mtandao wake wa
Twitter akisema hii ndio barua aliyoandika akiomba kustaafu.
Barua hiyo
aliyoandika Juni 18, 1974 iliwasilishwa kwa mwenyekiti wa Liverpool wa wakati
huo, JOHN SMITH akisomeka kwamba , SHANKLY anaomba kustaafu kuifundisha
Liverpool haraka iwezekanavyo na
litakuwa jambo zuri kama klabu hiyo itaanza kuandaa mafao yake.
Maombi hayo yalikubaliwa
na Smith Julai 12 mwaka huo ambapo aliitisha mkutano na waandishi wa habari
akisema kuwa Liverpool imepokea maombi ya ya kujiuzulu kwa kocha wao na bodi ya
klabu imekubali, huku akimshukuru kwa mchango mkubwa aliotoa Anfield.
SHANKLY, aliyeanza
kuifundisha Liverpool mwaka 1959, alishinda makombe matatu ya ligi daraja la
kwanza, mataji mawili ya FA na komba la UEFA, huku akiifanya Liverpool itawale
soka la England miaka ya 70 na 80.
0 comments:
Post a Comment