MWAKA 2012, Azam FC waliweka rekodi ya kuingia Fainali ya
kombe la Kagame wakiifunga 2-1 AS Vita Club ya Congo DR katika mechi ya nusu
fainali iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar
es salaam.
Wakati huo ikiwa ni takribani miaka sita tu tangu kuanzishwa
kwake, Azam iliweza kuiondoa klabu kongwe ya AS Vita ambayo inatikisa soka la
DR Congo na iliwahi kushinda kombe la Afrika mwaka 1973.
Msimu mmoja kabla ya kukutana na Azam katika mechi hiyo, AS
Vita walichukua ubingwa wa Congo DR wakiwashinda wapinzani wao wakubwa, TP
Mazembe ambao walikuwa mabingwa wa Afrika 2009 na 2010.
Kipute hicho cha nusu fainali kilikuwa kikali mno ambapo AS
Vita walianza kufunga goli la kuongoza dakika ya 35 kupitia kwa Alfred Mfongang akiachia shuti kali umbali wa mita 30 kutoka
kwenye eneo la hatari kufuatia kumzidi maarifa mlinzi wa Azam, Said Mourad.
Dakika ya
39, beki wa AS Vita, Issama Mpeko alionyeshwa kadi ya pili ya njano. Tukio hili
lilikuwa baya kwa mwamuzi wa kati, Dennis Batte kutoka Uganda kwani alishindwa
kugundua kwamba Mpeko alitakiwa kupewa kadi nyekundu.
Mpeko alicheza
kwa dakika tatu kabla ya Batte kugundua kwa msaada wa waamuzi wasaidizi.
Licha ya kufungwa
goli hilo, Azam walikuwa na matumaini ya kusawazisha na hawakubweteka kwasababu
wapinzani wao wamebaki 10. Walijua wana dakika nyingine 45 za kuandika rekodi.
Erasto Nyoni
alipiga krosi maridadi ambayo ilimaliziwa kwa kichwa na Nahodha John Bocco akiisawazishia
Azam dakika ya 68.
Dakika mbili
baadaye, Azam walifunga goli lingine la kichwa kutokana na mpira wa kona,
lakini mwamuzi alilikataa akidai
golikipa Nelson Lukong amesukumwa.
Azam waliendeleza
mashambulizi langoni mwa Vita na kwa mara ya kwanza katika mashindao ya mwaka
huo, Wacongo walionekana kubanwa tofauti na mechi zote walizocheza kuanzia
hatua ya makundi.
Licha ya
kukaza kwa zaidi ya saa ya mchezo, dakika ya 88, Mrisho Ngassa aliwaacha mabeki wa Vita na kuiwahi
pasi ya Abubakar Salum 'Sure Boy' na kuandika bao la pii.
Kocha wa AS
Vita , Medard Lusadisu alikubali kushindwa na akalisifu soka la ukanda wa
Afrika mashariki na kati.
Hakuweza
kujitetea kwasababu ya kadi nyekundu akisema: "Ukipata kadi ya pili ya
njano unatolewa kwa kadi nyekundu, ndivyo ilivyo. Tumejifunza mengi kutoka
mpira wa CECAFA, upo kiwango cha juu sana".
Kumwagiwa
sifa na klabu maarufu ya AS Vita inayopambana na timu zilizofanikiwa katika
soka la Afrika kama vile TP Mazembe, DC Motema Pembe lilikuwa jambo la faraja
kwa CECAFA.
Kocha wa
Azam fc, Stewart Hall alisema ni mafanikio makubwa kufika fainali.
"Wamiliki
wa timu hii (Azam fc) wanataka kuweka historia katika soka na biashara kwa
ukanda wa Afrika mashariki na kati pamoja na Afrika nzima. Nadhani sisi watu wa
mpira tupo njia sahihi kuwasaidia kufanikisha nia yao"
Kocha huyo
aliyekuwa na furaha alisema anaangalia mechi ya fainali ambapo alimsubiri
mpinzani kutoka katika mechi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya APR
kutoka Rwanda.
Stewart
alisema: "Sitaiangalia mechi hiyo! sijali nani atashinda".
Yanga
walishinda 1-0 dhidi ya APR, goli
likifungwa na Hamis Kiiza dakika ya 100.
Wakakutana
na Azam katika mechi ya fainali ambapo mabao mawili ya Kiiza na Said Bahanuzi yaliwapa
ushindi wa 2-0 dhidi ya Lambalamba na kuweza kutetea ubingwa.
Ikiwa
imepita miaka takribani mitatu sasa, Azam leo wanaingia kucheza nusu fainali ya
pili ya Kombe la Kagame dhidi ya KCCA ya
Uganda katika uwanja ule ule uliotumika mwaka 2012 dhidi ya AS Vita na kocha ni
yule yule, Stewart Hall.
Mechi ya
kwanza ya kundi C, Azam waliifunga KCCA 1-0 , goli la John Bocco ambaye pi alifunga
goli katika nusu fainali ya mwaka 2012 dhidi ya AS Vita.
Je,
histori ya nusu fainali ya 2012 inaweza kujirudia uwanja wa Taifa?...Tusubiri
dakika 90 au 120....
0 comments:
Post a Comment