Sunday, July 26, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
YANGA na Azam FC zitakumbushia fainali ya 2012 ya Kombe la Kagame zitakapomenyana kwenye Uwanja wa Taifa keshokutwa Jumatano baada ya leo jioni Wanajangwani kuibuka na ushindi wa baio 1-0 dhidi ya Al Khartoum FC.
Mechi hiyo ya mwisho ya Kundi A imechezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia Yanga ikianza na wachezaji wawili ambao hawakucheza kabisa mechi tatu za awali za kundi hilo, mabeki Oscar Joshua na Pato Ngonyani pamoja na mchezaji aliyekuwa akianzia benchI, kiungo Andrey Coutinho.
Kwa matokeo hayo, Yanga imemaliza nafasi ya pili Kundi A ikiwa na pointi tisa, moja nyuma ya vinara Gor Mahia ya Kenya ambayo itamenyana na 'Best Looser'.
Timu hiyo ya Jangwani sasa itamenyana na Azam FC Jumatano katika hatua ya mtoano ya robo fainali.
Mshindi wa tatu wa Kundi A, Al Khartoum atachuana na APR FC ya Rwanda kesho katika hatua hiyo ya robo fainali.
Hadi mapumziko Yanga wakikuwa mbele kwa goli 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wao hatari kutoka Burundi, Amissi Tambwe aliyemalizia kwa kichwa mpira wa kona iliyopingwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima 'Fabregas' kutoka Kaskazini Magharibi mwa Uwanja wa Taifa dakika moja kabla ya nusu saa ya mechi.
Al Khartoum walicheza kwa nidhamu kubwa kipindi hicho cha kwanza wakiwaruhusu Yanga kupiga mashuti matatu tu dakika za 15, 34 na 41. 
Shuti la mguu wa kulia mshambuliaji Malimi Busungu dakika ya 15 na lile la tikitaka la Tambwe dakika ya 34 ndiyo yaliyolenga lango na kupanguliwa na mabeki wa timu hiyo ya Sudan huku winga wa kushoto Mbrazil Andrey Coutinho akipaisha dakika nne kabka ya mapumziko.
Wasudan hao walipiga mashuti 11 kipindi hicho cha kwanza dakika za 5, 8, 14,16, 24, 28, 30, 31, 36, 44 na 45, lakini wapigaji wao Domenic Abul, Atif Khalif na Wagdi Awad hawakuwa na bahati ya kufunga kwani mipira yao ilishia kudakwa na kupanguliwa na kipa Ali Ali Mustafa 'Barthez' au kuokolewa na mabeki Kelvin Yondani na Pato Ngonyani.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Yanga wakimtoa beki wa pembeni kushoto, Oscar Joshua ambaye muda wote alikuwa akizomewa na mashabiki wao, nafasi yake ikachukuliwa na beki wao mpya Mwinyi Haji huku Al Khartoum ikimtoa Atif Khalif na pengo lake kuzibwa na Ismail Baba.
Ndani ya dakika 20 za kipindi hicho cha pili, Yanga walipata nafasi mbili nzuri za mabao lakini Tambwe akapaisha ndani ya boksi akishinda kuitendea krosi safi ya winga wa kulia Simon Msuva dakika ya 55 huku winga huyo naye akimwangusha Tambwe kwa kupaisha kwa guu lake la kulia alipojaribu kumalizia krosi ya Tambwe iliyotua ndani ya boksi dakika tano baada ya saa ya mchezo.
Beki wa mpya pembeni kulia, Joseph Zutah naye aliwafanya mashabiki wa Yanga washike vichwa baada ya kupaisha ndani ya boksi alipojaribu kuunganisha kwa mguu wa kulia krosi maridhawa iliyotua kutoka wingi ya kulia alikokuwa Msuva dakika 10 baada ya saa ya mchezo.
Mguu wa kushoto ulimfanye Tambwe ashike kichwa katika dakika ya 77 baada ya shuti lake la ndani ya boksi kupanguliwa na kipa Mohamed Ibrahim baada ya kupewa pasi na Msuva.
Dakika mbili baadaye kipa Barthez alifanya kazi ya ziada kupangua shuti la ndani ya sita lililopigwa na mshambuliaji Amin Ibrahim aliyewatoka mabeki wa Yanga kabla ya kukunjuka kwa mguu wa kulia.
Katika dakika ya 84 Tambwe pia alipiga ngumi chini kisha kukaa na kuinama baada ya kupaisha alipokuwa akimalizia krosi ya kiungo mtokea benchi Godfrey Mwashiuya kutoka wingi ya kushoto kusini mwa Uwaja wa Taifa.
Kichwa cha beki wa kati aliyetoka benchi, Nadir Haroub 'Cannavaro' hakikulenga lango pia alipokuwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Niyonzima dakika mbili kabla ya mechi kumalizika.
Vikosi vilikuwa:
Al Khartoum: Mohamed Ibrahim, Amin Ibrahim, Hamza Daoud, Salaheldin Mahamoud, Samawal Merghani, Wagdi Awad/ Salah Eldin (dk. 57), Antony Akumu, Domenic Abul, Atif Khalif/ Ismail Baba (dk. 47), Badreldin Eldoon/ Marwan Salih (dk. 62) na Ahmed Adam.
Yanga: Ali Mustafa, Joseph Zutah, Oscar Joshua/ Mwinyi Haji (dk. 46), Pato Ngonyani, Kelvin Yondani/ Nadir Haroub (dk. 83), Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Andrey Coutinho/ Godfrey Mwashiuya (dk. 65).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video