Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Donald Ngoma ameondoka nchini kurejea kwao Zimbabwe kwa ajili ya kuagana na timu yake ya zamani FC Platinum kabla kurejea nchini Jumapili kwa ajili ya kuanz kuitumikia rasmi timu ya mabingwa mara 25 wa Tanzania Bara.
Mtandao wa Goal.com umemnukuu Ngoma akieleza kuwa amefurahi kujiunga na Yanga na atahakikisha anacheza kwa kujituma ili aweze kuweka historia ya kuwa mmoja wa waliochangia mafanikio katika timu hiyo.
“Ninakwenda nyumbani kwa siku tatu, Jumapili nitarudi kwa ajili ya kuendelea na mazoezi Jumatatu, ninataka kwenda kuaga na kuchukua vifaa vyangu vingine ikiwamo familia. Mashabiki wa Yanga watarajie mambo makubwa kwangu,” amesema Ngoma.
Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga na hiyo imetokana na rekodi yake nzuri aliyoionesha wakati akiichezea FC Platinum chini ya kocha Norman Mapeza.
0 comments:
Post a Comment