Mshambuliaji mpya waklabu ya Yanga Donald Ngoma leo ameanza vyema kwenye mechi yake ya kwanza baada ya kuifungia klabu hiyo goli pekee kwenye ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya KMKM ya Zanzibar mchezo uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa Taifa.
Ngoma alifunga goli hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Andrey Coutinho dakika ya 50 ya mchezo.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kujipima nguvu kwa timu zote mbili kuelekea kwenye michuano ya Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi Julai 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo timu hizo (Yanga na KMKM) zote zipo kwenye kundi moja na zitakutana kwenye michuano hiyo kwenye hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment