Beki wa kati wa Malakia FC ya Sudan Kusini Yengo Song Ngum ni mchezaji wa kimataifa wa Cameroon anaekipiga kwenye ligi kuu ya Sudan Kusini ambaye kwa sasa yupo na klabu yake jijini Dar es Salaam kwenye michuano ya Kagame Cup inayoendelea kusonga mbele.
Song ambae ametoka kijiji kimoja na mchezaji na nahodha wa zamani wa Cameroon Rigobert Song amejiunga na Malakia Januari mwaka huu akitokea DCMP ya Kinshasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Song amesema, mashindano ya Kagame ni mazuri kwasababu yanatoa nafasi kwa wachezaji kuonekana na kujulikana sehemu nyingine zaidi ya wanapocheza kwenye ligi za ndani lakini pia inatoa uzoefu kwa wachezaji kwasababu wanakutana na timu nyingi kutoka sehemu mbalimbali za ukanda huu wa Afrika wa Mashariki na Kati.
“Mashindano haya ni mazuri kwasababu yanatoa nafasi kwa wachezaji kuonekana na timu nyingine na makocha wanafuatilia vizuri michuano hii huwezi jua unaweza kupata timu nyingine ambayo inaweza kukusajili na kukupa maslahi mazuri kuliko timu unayocheza wakati huu”, alisema.
“Ukiachana na uwezekano wa kupata timu nyingine, vilevile mashindano haya yanajenga uzoefu kwa wachezaji kwenye mechi za kimataifa. Michuano hii inakutanisha timu kutoka nchi mbalimbali hapa unaweza kupata uzoefu utakaokusaidia ukiwa unacheza kwenye mashindano mengine makubwa kama klabu bingwa Afrika na kombe la sirikisho”, amesisitiza.
Alipoulizwa ni kitu gani ambacho amekifurahia tangu amefika Tanzania Song alisema; “Hapa kuna amani sana yani toka tumefika hapa tumeshangwazwa na amani iliyopo hapa maana watu wanazunguka usiku mzima lakini ukiwa Sudan ikifika saa mbili usiku watu wote wanakuwa wameshajifungia ndani na kama unazunguka usiku basi basi utakuwa unatafuta matatizo”,lisema.
Song amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itavutiwa nae kikubwa kwake ni maslahi na kama watafikia makubaliano yeye yuko tayari kukipiga kwenye timu yoyote.
Mkali huyo alikuwa nguzo imara wakati timu yake ikipata ushindi mbele ya Adama City ya Ethiopia lakini pia aliongoza vyema safu yake ya ulinzi wakati timu yake ilipokabiliana na Azam FC wakiweza kuhimili mikikimikiki ya washambuliaji wa ‘wanalambalamba’ John Bocco, Ame Ali na Kipre Tchetche japo walipoteza mchezo huo kwa goli 2-0.
0 comments:
Post a Comment