Monday, July 13, 2015

Kocha wa klabu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba amesema anataka kuongezwa kwa golikipa mwingine kwasababu Ivo pekeyake ameonekana hatoshi huku kocha huyo akiongeza kwamba, magolikipa wengine wa kikosi hicho bado hawajaiva kuwa tayari kuhimili mchakamchaka wa ligi kuu.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Hans Poppe amethibitisha kuwa timu yao inahitaji golikipa mwingine na huenda watatumia mashindano ya Kagame ili kupata kipa atakae jiunga na klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
“Sisi bado tunaendelea, bado tunahitaji golikipa kutokana na maagizo ya kocha, Ivo pekeyake hatoshi kama akiumia tutapata shida na hawa wengine hawajaiva sawasawa kuwa wachezaji wakuaminika kwenye kikosi cha kwanza, kwahiyo wanahitaji muda wa kuendelea na mazoezi na mafunzo kadha wa kadha”, amesema Hans Poppe.
“Timu inatakiwa kuwa na kipa ambaye yuko tayari kama alivyo Ivo, maana kuna kuugua, kuna kuumia na kuna kadi tatu za njano na kadi nyekundu. Sasa yote haya au mojawapo linaweza likamsibu kipa tuliyenae halafu tukashindwa kuwa na mbadala”, ameongeza.
“Kuhusu kipa, tunaangalia sehemu nyingi. Kuna Kagame Cup inakuja hapa tutaangalia tunaweza tukaibuka na kipa hapahapa”, alimaliza.
Golikipa anaechipukia kutoka ndani ya klabu hiyo Manyika Jr, ameshindwa kuaminiwa baada ya kudaiwa kiwango chake kushuka tofauti na alivyoanza ambapo baadhi ya wadau wa soka walianza kumtabiria makubwa kwenye klabu hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video