YANGA SC imeshinda 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibout katika mechi ya pili ya kombe la Kagame iliyopigwa leo jioni uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Moja ya stori kubwa ni mzimu wa kukosa penalti kwa wachezaji wa Yanga, kwani katika mechi mbili wamekosa penalti tatu.
Mechi ya kwanza ambayo walifungwa 2-1 na Gor Mahia, nahodha wa klabu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro' alipiga penalti aina ya Panenka ambayo ilidakwa na Golikipa Boniface Oliochi.
Leo Simon Msuva na Amissi Tambwe wamekosa penalti na kuwashangaza wengi.
Kutokana na hali hiyo, kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa ameulizwa kwanini wachezaji wanakosa penalti?
"Tunashukuru Mungu tumeshinda, wachezaji walianza kwa papara, walitaka kufunga magoli ya haraka. Zile penalti tumeshangaa walivyokosa, kwenye mazoezi walifanya vizuri, wote walipiga vizuri. lakini leo wamekosa, inawezekana kwasababu ya tension ya mechi". Amesema Mkwasa.
0 comments:
Post a Comment