Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF na makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Said Mohamed leo amefungua kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika ofisi za TFF zilizopo Karume.
Katika ufunguzi wa kozi hiyo, Said amesema anashukuru FIFA kwa kuwapa nafasi ya kuendesha mafunzo hayo ya makocha wa makipa kwa mara ya kwanza nchini, na kuwaomba washiriki wa kozi hiyo kutumia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Jumla ya makocha 31 wanashiriki kozi hiyo kutoka vilabu vyote viliyovopo Ligi Kuu na magolikipa wa zamani waliodakika timu za Taifa.
Kozi hiyo ya makocha wa makipa inaendeshwa na mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka nchini Ufaransa, ambapo kozi hiyo itafungwa rasmi tarehe 17 Julai mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment