Alex Morgan amekuwa mwanamke wa kwanza kutokea kwenye Cover ya Video Game ya FIFA.
Mshambuliaji huyo wa Marekani alifanya kazi kubwa ya kuipa ubingwa nchi yake katika fainali za kombe la dunia la Wanawake lililofanyika mwaka huu nchini Canada, ingawa Carli Lloyd alitishia kuchukua nafasi yake.
Lloyd alipiga Hat-trick ya kwanza katika historia ya kombe la dunia dhidi ya Japan kwenye mechi ya fainali.
Morgan ndiye mwanamke pekee kutokea kwenye Cover ya Video Game za FIFA toleo la FIFA 16 sambamba na mchezaji nyota wa Dunia, Lionel Messi.
Nahodha wa Canada, Christine Sinclair, mshambuliaji chipukizi wa Australia, Stephanie Catley, nao wataingia kwenye Covers.
Huu ni mwaka wa kwanza ambao Gamers watacheza Video game za Wanawake ikitokana na mafanikio makubwa ya fainali za mwaka huu.
Tazama picha za Covers hapa chini.....
0 comments:
Post a Comment