Wednesday, July 1, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KLABU ya Simba imefanya kweli tena baada ya leo kuzindua kadi mpya za uanachama ambazo zitatoa fursa kwa watakaojiunga kunufaika na bima ya maisha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kadi hizo jijini Dar es Salaam leo mchana, Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, amesema kila mwanachama atakayejiunga na kuchukua kadi mpya, atapata bima ya maisha inayojulikana kwa jina la 'Simba Pamoja'.

Amesema bima hiyo itampatia mwanachama ambaye amelipa malipo yake ya mwaka ya uanachama fedha taslimu zisizopungua Sh. 250,000 ikiwa atapata msiba kwa kufiwa na mtoto, mke ay yeye mwenyewe.
Aveva amesema malipo ya uanachama hayajabadilika na yanaendelea kuwa Sh. 1,000 kwa mwezi, hivyo mwanachama atalipa ada ya mwaka Sh. 12,000 kwa wanachama hai na Sh. 30,000 kwa wanachama wapya.

“Hii ndiyo klabu pekee Afrika Mashariki na Kati inayotoa fao hili kwa wanachama wake, Simba inajali sana wanachama wake na tutaendelea kuimarisha uhusiano wa klabu na wanachama,” amesema Aveva.

Aveva ambaye alikuwa amefuatana na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya EAG Group, Imani Kajula, pia amezindua kadi ya Simba kwa ajili ya watoto wanaoipenda timu hiyo 'Simba Cub Membership Card' ili kuwawezesha kutambuliwa na kuwa wanachama wa timu hiyo.

“Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto siyo tu kutambuliwa kuwa wanachama wa Simba, bali kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio yanayoandaliwa na Simba na kwenye maduka (yanayouza bidhaa za Simba) pia yatatoa punguzo kwa watoto wenye kadi hizo,” amesema.

Kajuna amesema upatikanaji wa kadi hizo ni moja ya majukumu ya kampuni yao waliyoingia na klabu ya Simba kuhakikisha wanabuni mbinu zitakazoisaidia klabu hiyo kupata mapato.
Alisema wanachana wanaohitaji kujiunga wanatakiwa kutuma maombi ya kupata kadi kupitia tovuti ya klabu hiyo ya www.simbasport.co.tz.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video