Saturday, July 11, 2015


Na Ramadhani ngoda.
Mcheza Tenisi namba 3 kwa ubora ulimwenguni na nambari moja nchini Uingereza, Andy Murray amefutiwa ndoto za ubingwa wa pili wa michuano ya tenisi ya Wimbledon baada ya kucharazwa na bingwa mara 7 na nyota nambari mbili kwa ubora, Roger Federe kwa seti  7-5 7-5 6-4 katika mchezo wa nusu fainali na kuwaacha Waingereza katika majonzi kwani sasa ni wazi taji hilo linatoka nje ya ardhi hiyo kwa mara nyingine.

Federer (33) anakuwa ni mchezaji mkubwa Zaidi kutinga fainali tangu Muaustralia, Ken Rosewall aliyekuwa na umri wa miaka 39 wakati huo kufanya hivyo mwaka 1974, na sasa atavaana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Novac Djokovic katika hatua ya fainali siku ya Jumapili (Julai 12).

Murray ambaye tayari alishapoteza mara mara 3 dhidi ya Federer, alikuwa na nafasi ya kupindua rekodi hiyo hasa katika mchezo wa tano wa kota ya kwanza alipoonekana mwenye nguvu na kasi kwa kupiga mipira ya hatari na hiyo kuwa nafasi pekee kwa Muingereza huyo.

Matokeo hayo yanaonesha kutoshtua wengi hasa kutokana na takwimu kumuhukumu Murray dhidi ya Federer ambaye ameshashinda 93% ya maisha yake ya tenisi licha ya kuwa tayari alishamburuza mara 3 Muingereza huyo.

Kama ilivyo ada, Federer alikiri kupata upinzani mkubwa katika mchezo huo licha ya kuibuka na ushindi uliomkatia tiketi ya fainali ya michuano hiyo inayofanyika nyumbani kwa mpinzani wake.

“Ilikuwa ngumu sana. Mekuwa akicheza vizuri sana msimu mzima,” alisema Federer baada ya mchezo huo.

“Nina furaha isiyoelezeka. Nimecheza vizuri sana katika kipindi chote nap engine inaweza kuwa sababu ya kushinda. Nimekuwa napiga mipira yangu ya kwanza vizuri, niliweka shinikizo (kwa wapinzani wake), nilikuwa nikishuti na nimeweza kufanya yote kama ambavyo nimekuwa nikifanya. Kila kitu kilikwenda sawa,” aliongeza Mswiss huyo.

Murray kwa upande wake alikubali kuzidiwa uwezo na mpinzani wake licha yay eye naye kucheza kadri alivyoweza ili kulinda heshima ya nchi yake.

“Nimecheza vizuri lakini yeye (Federer) amecheza vizuri Zaidi,” alisema Murray baada ya mchezo.





0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video