Sunday, July 12, 2015

Baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga, mchezaji Simon Msuva amesema ndoto yake ya kucheza soka la kimataifa bado ipo palepale. Kinara huyo wa mabao na mchezaji bora wa msimu uliopita amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwaunga mkono wachezaji wote wapya na wale wa zamani.
“Wakati ninao, nia ninayo, naamini kwa uwezo wa Mungu ndoto yangu haitoweza kuvunjika  kwasababu Yanga ni timu yangu najihisi nipo nyumbani na Yanga siyo mwisho wa safari yangu. Kunakipengele kwenye mkataba iwapo nitapata timu nje wataniruhusu niende, kama nitafanikiwa watakubaliana wao kama wao”, amesema Msuva.
“Ile timu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini ilifikia hatua wakataka kutoa kiasi flani lakini Yanga wakawaambia hatujaridhia tunataka kiasi flani kwahiyo ikawa ngumu kwasababu hawakufikia maridhiano ikabidi mimi niendelee kubaki”, amefafanua.
“Kwanza mimi nashukuru kwa uwezo wa Mungu amepatikana kocha ambaye ameweza kuifundisha timu mpaka imefikia sehemu ile, kaweza kutumia wachezaji vizuri kwa wakati. Pia nawaomba mashabiki waendelee kuwa na imani na timu yao, kunawachezaji wapya wanahitaji kuwapa sapoti ili kwa pamoja tuendelee kufanya vizuri na klabu yetu”, ameongeza.
Mwishoni mwa msimu uliopita, Msuva alienda kwenye klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na kikosi hicho lakini muda mrefu ukapita bila kujua nini hatma ya winga huyo kama alifuzu au alishindwa kwenye majaribio mpaka alipoamua kufafanua mwenyewe kwamba, dili hilo lilishindikana kwasababu vilabu vyote viwili havikufikia makubaliano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video