Friday, July 17, 2015

Kocha wa Yanga SC Hans van der Pluijm (kulia) akiwa na kocha wa Gor Mahia Frank Nuttal (kulia) walipozungumza na Waandishi wa Habari mchana huu

Makocha wa timu za Yanga na Gor Mahia ya Kenya wamezungumzia mchezo wao wa kesho ambao ndio utakuwa mchezo wa ufunguzi kwenye michuano ya Kagame Cup mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 10:00 za jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Kila kocha ametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa ni mkali kutokana na ubora wa vikosi vya timu zao. 
Yanga ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara ambayo ilimalizika mwezi Mei mwaka huu wakati wapinzani wao wakiwa wanaongoza ligi ya Kenya inayoendelea kutimua vumbi nchini humo.
Van Pluijm 1Kocha wa mkuu wa Yanga Hans Van Pluijm amesema anawaheshimu sana wapinzani wake timu ya Gor Mahia lakini hawaogopi na anamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
“Nimekuwa Afrika tangu mwaka 1996 hivyo ninauzoefu na soka la timu za hapa kwa muda mrefu, tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuikabili kila timu kwenye michuano hii. Kitu kikubwa ni kwamba, mimi huwa sidharau mpinzani wangu kwasababu kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna mtu anayejua matokeo”, amesema Pluijm.
Kocha mkuu wa Gor Mahia Frank Nuttal akizungumza na waandishi wa habari
Kocha mkuu wa Gor Mahia Frank Nuttal akizungumza na waandishi wa habari
Kwa upande wake kocha mkuu wa Gor Mahia Mcotish  Frank Nuttal amesema yeye hana uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake (Van Pluijm) lakini akasisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili Yanga kesho kwenye uwanja wa Taifa.
“Yanga ni timu kubwa japo sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu yenye ushindani na mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo tutajua matokeo”, amesema kocha huyo.
Van Pluijm 2Mchezo mwingine wa kundi A utachezwa kwenye uwanja wa Karume ukizikutanisha KMKM dhidi ya Telecom kutoka Djibouti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video