Taarifa zinasema kuwa, klabu ya Manchester United imeanza kusaka mshambuliaji kwa ajili ya kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye ameshajiunga na kikosi cha Fenerbahce na mtu anayewekwa kwenye rada ya Machester United ni mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya Ubelgiji Christian Benteke.
Van Gaal yuko tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 32.5 ili kumnasa mkali huyo imeripotiwa na The Daily Mail. Mkataba wa Benteke unakipengele kinachomruhusu kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayofikia dau la pauni milioni 32.5 na inasemekana Man United wanataka kumsajili mshambuliaji mwenye jina kubwa katika kipindi hiki.
United imeshawanasa Bastian Schweinsteiger, Matteo Darmian na Morgan Schneiderlin inaonekana inataka kukiboresha kikosi chake kwenye kipindi hiki cha usajili wakati huo ikiwa imesha msajili pia Memphis Depay.
0 comments:
Post a Comment