Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameanzisha mashambulizi kwa kocha wa Real Madrid Rafael Benitez, akisema kuwa aliiharibu timu yake ya Inter na kumdhihaki kwa uwezo wake mdogo wa kufundisha.
Mke wa Benitez, Montserrat Seara, alileta mtikisiko wakati aliposema kuwa mara zote mume wake amekuwa akifanya vyema sehemu zote ambazo Mourinho amepita huku akitolea mifano timu za Inter, Chelsea and na sasa Madrid ambapo kote humo Mourinho amewahi kuwa kocha.
Mourinho naye hakuwa nyuma badala yake ameamua kurudisha mashambulizi kwa kusema.
"Nahisi huyu mwanamke atakuwa amechanganyikiwa kwa namna fulani hivi", Mourinho alisema baada ya ushindi wa penati wa magoli 4-2 dhdi ya Barcelona baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.
"Sicheki. Kwa sababu mume wake alienda Chelsea kumrithi Roberto Di Matteo na pia ameenda Madrid kumrithi Carlo Ancelotti.
"Klabu ambayo mume wake amerithi kutoka kwangu ni Inter Milan tu, ambapo kwa takribani muda wa miezi sita tu aliiharibu timu ambayo ilikuwa bora Ulaya kwa kipindi hicho.
"Na kwa upande wake nadhani kufikiri kuhusu mimi ni kuongea kuhusu mimi, Mimi nadhani yule mama anahitaji kuutumia muda wake vizuri kumhudumia mume wake na kwa kufanya hivyo nahisi atakuwa na fursa finyu sana kuongea kuhusu mimi".
0 comments:
Post a Comment