Meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa huenda akaondoka katika kilabu ya Manchester United mwisho wa kandarasi yake ya miaka mitatu ili kutimiza ahadi aliyotoa kwa mkewe.
Alipoulizwa iwapo ataongeza kandarasi yake kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Old Traford ,raia huyo wa Uholanzi ameiambia BBC kwamba ataondoka mwisho wa kandarasi yake mwaka 2017.
''Nilimuahidi mkewe wangu.hatuna miaka mingi iliosalia,na hiyo ndio sababu'', alisema meneja huyo mwenye umri wa miaka 63.
''Nimefanya kila kitu katika maisha yangu kama mkufunzi''.
Alipulizwa iwapo kuna uwezekano wa yeye kusalia katika klabu hiyo,alijibu kwamba hawezi kutoa jibu lolote kwa kuwa mkewe amekasirika sana.
Alipulizwa iwapo kuna uwezekano wa yeye kusalia katika klabu hiyo,alijibu kwamba hawezi kutoa jibu lolote kwa kuwa mkewe amekasirika sana.
''Nakiri kwamba nilimwambia kuwa ningestaafu ifikiapo miaka 55 lakini mapaka sasa nikiwa na umri wa miaka 63 bado naendelea na ukufunzi na wiki ijayo natarajia kufikisha miaka 64''alisema meneja huyo.
0 comments:
Post a Comment