Thursday, July 9, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KATIKA safu hii ya wasifu wa mchezaji, leo tunamwangalia mshambuliaji hatari Saad Kipanga wa JKT Ruvu Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Felix Minziro.

DONDOO ZA KIPANGA
Kuzaliwa: Julai 5, 1990 
Umri: Miaka 25
Mahali: Nzega, Tabora
Klabu alizocheza: African Lyon, Rhino Rangers, Mbeya City, Police Tabora na Royal de Muramvya ya Burundi.
Baba yake: Halfan Kipanga
Mke wake: Therezia Mashaka 
Mtoto wake: Zuena

Kama ilivyo kwa Amour Omary Janja, ambaye pia ametua JKT Ruvu akitokea JKU ya Ligi Kuu ya Zanzibar, Kipanga naye ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya nje ya boksi na ana kasi katika kukimbia.

Kipanga (25) aliwahi kuzitumkia klabu mbalimbali zikiwamo African Lyon, Rhino Rangers, Mbeya City, Police Tabora na Royal de Muramvya ya Burundi.

Ni mchezaji pekee wa VPL kwa sasa aliyewahi kuifunga Simba mabao matatu katika mechi tatu mfululizo. alipofanya hivyo mwaka juzi (2013) 

Ni Mfungaji Bora wa FDL msimu wa 2012/13 akiziona nyavu mara 12 katika mechi 14 akiwa na kikosi cha Rhino Rangers ya Tabora.

Kusajiliwa kwa mume huyo wa Therezia Mashaka na baba wa Zuena katika kikosi cha JKT Ruvu ni ishara kwamba Minziro amedhamiria kufanya kitu kikubwa msimu huu.

Uwezo wake wa kukimbia kwa kasi, kukaba na mashuti yake makali ni moja ya sifa zilizomfanya awe lulu katika kikosi hicho cha Rhino Rangers kilichokuwa chini ya kocha aliyetimuliwa msimu wa 2013/14 wa VPL, Sebastian Nkoma.

Ni mshambuliaji hatari, ambaye mabeki wote VPL hawana budi kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanamchunga asipate hata nafasi moja ya kupiga shuti kwani kosa moja kwa mkali huyo litazigharimu timu zao.

Kipanga aliifunga Simba katika mechi tatu mfululizo ambazo Rhino na Simba zilikutana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mwaka jana. Katika mechi ya kwanza ambayo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kwenye uwanja huo uliojengwa 1987, Kipanga ndiye aliifungia bao Rhino katika dakika ya 43 akisawazisha bao la penalti lililofungwa na Ramadhani Singano 'Messi' dakika ya 35.

Julai 9, 2013 mshambuliaji huyo wa zamani wa Klabu ya Royal FC de Muramvya inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi, pia alifunga bao pekee la Rhino katika mechi yao ya pili ya kujiandaa kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara waliyolala 3-1 dhidi ya 'Wanamsimbazi' kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuketisha watazamaji 30,000.

Mzaliwa huyo wa Nzega, Tabora ndiye aliyefuta ndoto za Simba kuuanza msimu wa 2013/14 kwa ushindi baada ya kuifungia timu yake bao la pili na la kusawazisha kwenye mechi yao ya ufunguzi iliyomalizika kwa sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora Agosti 24, 2013.

CHIMBUKO LAKE KISOKA
Kipanga aliyezaliwa Julai 5, 1990 Nzega, Tabora, anasema alianza kusakata soka akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nyasa One (1) iliyopo Nzega (2000- 2006) na kwamba kipaji chake kilionekana zaidi 2007 alipojiunga na shule ya sekondari Tarime ya mkoani Mara.

"Nikiwa kidato cha pili 2008 nilishiriki michuano ya Copa Coca-Cola nikiwa na timu ya Mkoa wa Tabora. Baada ya mashindano hayo kumalizika, nilichaguliwa kujiunga na kikosi cha kocha Sylivester Marsh cha timu ya taifa ya vijana chini umri wa miaka 17 (U17)," anasema Kipanga.

"Nakumbukua tulikwenda Sudan kushiriki mashindano ya U17 ya Cecafa (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) na tuliporejea nilijiunga na kikosi cha U-20 cha African Lyon wakiniahidi kunipeleka kwenye shule ya vipaji ya michezo ya Makongo, lakini ilishindikana na ikabidi nirudi Tarime," anaongeza.

Mtoto huyo pekee kwenye familia ya Halfan Kipanga, anasema baada ya kupata alama zisizoridhisha kwenye mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2010, ilibidi ategemee soka kuendesha maisha yake.

Anasema 2011 alishiriki mashindano ya Taifa Cup akiwa na timu ya Mkoa wa Tabora na kwamba baada ya mashindano hayo alianza kukipiga katika Ligi Kuu ya Burundi akiwa na Klabu ya Royal FC de Muramvya.

"Nawajua vizuri Amisi Tambwe (Simba) na Didier Kavumbagu (Yanga) kwa sababu nimecheza nao Burundi ingawa nilicheza kwa nusu msimu (miezi sita) nikaamua kurejea nyumbani baada ya kukubaliana 'vitu' vizuri na uongozi wa Rhino," anasema.

Kipanga, ambaye pia hupenda kucheza mpira wa kikapu, aliifungia Rhino mabao matano katika mzunguko wa kwanza wa VPL msimu wa 2013/14 na hakuwika sana kutokana na majeraha yaliyomkumba katikati mwa mzunguko huo kisha mzunguko wa pili akatua Mbeya City ambako alifunga mabao matano pia.

MAISHA BINAFSI
Kipanga, ambaye 2012 alijiunga na Kikosi cha 821 KJ mkoani Kigoma kwa ajili ya mafunzo ya miezi mitatu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), anasema anachukia ulevi na ugomvi.

Ana mke (Therezia Mashaka) na mtoto (Zuena). Anasema anapenda kukaa na familia yake wakati wa mapumziko wakila ugali na maharage huku wakishushia na juisi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video