Katika safu hii ya wasifu wa mchezaji anayecheza Tanzania, leo tunamwangalia Gaudence Mwaikimba. Mshambuliaji mrefu aliyezitumikia klabu kibao za Bongo.
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Dondoo za Mwaikimba
Kuzaliwa: Oktoba 5, 1984
Mahali: Kyela mkoani Mbeya
Umri: Miaka 30
Urefu: SM189
Klabu alizocheza: Tukuyu Stars (2003-2004), Kahama United (2004-2005), Ashanti United (2005-2006), Yanga (2006-2009), Sur (Oman, 2009-2010), Tanzania Prisons (2010-2011), Kagera Sugar (2011-2012), Moro United (2011-2012), Azam FC (2012-2015) na sasa JKT Ruvu.
MSIMU uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara haukuwa mzuri kwa Gaudence Mwaikimba (30) kutokana na kutopewa nafasi kubwa katika kikosi cha Azam FC kilichowategemea Mrundi Didier Kavumbagu na Muivory Coast Kipre Tchetche katika safu ya ushambuliaji.
Alifunga mabao matatu yaliyoipa Azam FC ushindi wa 2-1 (alifunga moja) dhidi ya Kagera Sugar FC na 4-0 (alifunga mawili) dhidi ya Stand United FC.
Akiwa kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara 2013/14, mshambuliaji huyo ambaye mara nyingi alianzia benchi, alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na kufunga mabao kwenye viwanja vibovu.
Mbali na kubebwa na urefu wa Sm189 na umbo kubwa la mwili, Mwaikimba aliyezaliwa Oktoba 5, 1984 Kyela mkoani Mbeya, ana uwezo mkubwa wa kukimbia na kupiga mashuti ya mbali.
Ukiziweka kando Azam FC na JKT Ruvu, Mwaikimba pia aliwahi kuzitumikia Tukuyu Stars (2003-2004), Kahama United (2004-2005), Ashanti United (2005-2006), Yanga (2006-2009), Sur (Oman, 2009-2010), Tanzania Prisons (2010-2011), Kagera Sugar (2011-2012), Moro United (2011-2012).
0 comments:
Post a Comment