Mshambuliaji wa Gor Mahia, Michael Olunga
Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga zinasema kwamba,
mshambuliaji wake, Rais wa Liberia, Kpah Sherman anakaribia kutua katika klabu
mojawapo inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.
Winga aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho anatafutiwa timu itakayomnunua
baada ya BDF XI ya Botswana kutaja pesa dau dogo la milion 10 za Kitanzania. Hata
hivyo St.George ya Ethiopia wameonesha kuvutiwa na Coutinho.
Yanga imepanga kumalizana na kiungo mkabaji wa Gor Mahia , Khalid
Auch pamoja na mshambuliaji Michael Olunga ambaye Azam FC na Simba SC wanawania
saini yake pia.
Beki kiraka, Mbuyu Twite yupo mashakani kuendelea kukipiga
Jangwani huku tatizo haswa imekuwa usumbufu kutoka klabu yake ya zamani ya FC
LUPOPO.
0 comments:
Post a Comment