Na Ramadhani ngoda.
Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Manchester
City imewawia kusubiri kabla ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Aston Villa,
Fabian Delph baada ya mkewe kukaribia kujifungua.
Delph ambaye amekamilisha asilimia kubwa ya
uhamisho wake kuelekea Etihad kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 8 na kufikia
makubaliano ya mkataba wenye thamani ya pauni 100,000 kwa wiki, anakwenda moja
kwa moja kuziba pahala palipoachwa na Muingereza mwenzake James Milner
aliyetimkia kwa majogo wa jiji Liverpool hivi karibuni.
Hii inamfanya Delph asijumuike mapema na City
katika maandalizi ya msimu mpya hasa safari ya timu hiyo ya nchini Australia
mpaka pale atakapokamilisha usajili wake uliobaki katika hatua ya vipimo vya
afya tu.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza kutoka Villa
Park ameahidiwa kupata nafasi kama aliyokuwa akiipata Milner katika kikosi
hicho kinachonolewa na Mchile Manuel Louis Pellegrini.
Delph anatarajiwa kuwa sehemu ya mpango wa
Manchester City wa kuongeza idadi ya wachezaji wazawa wakihitaji pia kwa udi na
uvumba saini ya winga mwingine wa kingereza Raheem Sterling kutoka kwa majogoo
wa jiji Liverpool kwani msimu uliomalizika ni Milner na aliyekuwa akicheza kwa
mkopo, kiungo Frank Lampard ndio wachezaji wazawa pekee waliopata nafasi ya
kuanza katika michezo Zaidi ya 10 katika michuano yote.
Katika hatua nyingine, ni kauli ya ‘kata mti panda
mti’ kwa Aston Villa ambao wameziba pengo la Delph kwa kumnasa kiungo wa Lille
Metropole ya Ufaransa, Iddrisa Gueye siku ya Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment