Tuesday, July 14, 2015

SOTE tumeanza kuijua kama Kagame Interclub Cup mnamo mwaka 2002, kipindi ambacha Rais wa Rwanda Paul Kagame alipoanza kuidhamini michuano hiyo inayoshirikisha vilabu bingwa kutoka Afrika Mashariki na Kati, mashindano haya yalianza mwaka 1967 na timu ya Abaluhya waliku mabingwa lakini haikuwa ikitambulika rasmi.
Mashindano Yalisimama mpaka mwaka 1974 ambapo Simba sc walipofanikiwa kuwa timu ya kwanza kuwa mabingwa kipindi ambacho michuano ilikuwa ikijulikana rasmi. Simba SC ndio klabu yenye mafanikio kuliko klabu yeyote kwenye mashindano hayo ikiwa imefanikiwa kuliweka kibindoni taji hilo mara 6, ikifuatiwa na mahasimu wao wa jadi vijana wa jangwani Young Africans SC iliyobeba taji hilo mara 5.
Wengi husema mafanikio ya yanga huichagiza simba sc kufanya vizuri au mafanikio ya simba sc huichagiza yanga sc kufanya vizuri, inawezekana ikawa hivyo kwani mwaka mmoja baada ya simba sc kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo mwaka uliofuata yaani 1975 Young Africans walifanikiwa kulitwaa taji hilo, maisha yaliendelea lakini historia ambayo wanajangwani hawataisahau ni ile ya kutwaa taji mara mbili mfululizo kwa miaka ya hivi karibuni yaani mwaka 2011 na 2012 huku mwaka 2012 Saidi Bahanuzi akiwa mfungaji bora wa mashindano kwa kuweka kambani goli 7, hakika ulikuwa mwanzo wa mafanikio kwa kijana huyu.
Yanga inakwenda katika mashindano hayo mwaka 2015 bila mfungaji wake bora wa mwaka 2012, nani ataibuka mfungaji bora wa mashindano mwaka huu?, je, atatoka tena yanga?
Wakati ukiendelea kuvuta picha tambua Tanzania inawakilishwa na timu tatu kama mwenyeji wa mashindano hayo, hapa nazizungumzia Azam FC, KMKM na Yanga .
Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Al Merreikh ya Sudan ambaye hata hivyo hatashiriki kutokana na kuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga imepangwa kundi A ikiwa na timu za Telecom Ya Djibouti, KMKM ya Zanzibar, Gor Mahia Ya Kenya na Khartoum ya Sudan.
Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al Ahly Shandy, LLB Ya Burundi, Elman Ya Somalia na Azam FC Ya Tanzania.
Hesabu zangu zinaniambia Azam FC baada ya kutolewa katika hatua ya robo mwaka jana, imejipanga ipasavyo mwaka huu ilikuweza kurudisha imani na thamani ya uwekezaji walioufanya, hakuna asiyefahamu Azam Complex Ulivyo uwanja wa kisasa. Michezo miwili ya kirafiki kule Tanga imetoa mwanga kwa mbali juu ya nuru iliyopo mbele ya safari.
Kule Jangwani sina shaka na kikosi chao kwani michezo minne ya kirafiki waliyocheza huku miwili ya mwisho wakiwa hawajaruhusu hata goli moja, kama sehemu ya maandalizi ya Kagame Cup imetoa mwanga pia, ushindi wa goli 3-0 dhidi ya kombaini ya polisi huku mfungaji bora wa ligi na mchezaji bora pia, Simon Msuva akiweka kambani goli moja . Ingizo jipya, Donald Ngoma aliendelea kutunisha akaunti yake ya magoli kwa kufunga bao la pili tangu ajiunge na wanajangwani.
Kama nilivyotangulia kusema, mafanikio ya Yanga huweza kutegemea yale ya Simba na kinyume chake. Baada ya Simba kuchukua mara 6, huenda Yanga nao wakatangaza ubingwa wa mara ya 6 kwani ndio nafasi adimu kwao kuamua kufanya hivyo kwani Simba hawatashiriki mwaka huu.
Chanzo: Sokatanzaniacom

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video